Welcome to Dr Cheni website!
Dr CheniDr CheniDr Cheni
(Sat - Fri)
Tanzania
Dr CheniDr CheniDr Cheni

Usiku mwingike mzuri tukisheherekea usiku wa Wakili msomi Derick na Mke wake Sellen katika ukumbi wa Primrose usikunulipendeza sana na wahaya walikuwa na shangwe kubwa sana kwa siku ya kijana wao ilikuwa ukigusa tu wahaya hao washainuka yani walijua sana kuichangamsha sherehe.

Ukumbini Derick na Mkwe wake Sellen waliingia ndani ya ukumbi kwa kupendeza sana na waka kama maraika maana bwana harusi suti nyeupe na shela la mke wake wakawa kama ndege wanaofanana na kuruka kwa pamoja.

Moja kati ya jambo ambalo nimelipata toka kwa baba yale na Derick ni mtu wa kujitoa sana kwa jamii hii ikasababisha sherehe kuwa na majirani ambao ukisema vigelegele tafadhari basi bila hata kupewa kipaza sauti vigelegele vitasikika ukumbi mzima bila kukwama kwama.

Maida wa siku ya Derick na Sellen ni kama vile walipania yani huko kucheza ni kama vile watavunjika muda si mrefu, na kuna kijana mmoja ambaye kwao mdo mfupi kuliko wote ni mwembamba lakini anacheza bila hata kuionea huruma mifupa.

Lakini waliipendezeasha sana siku ya Derick na hakika lazima hata kamati itaona kama kile kiasi walichowapa Maids hawa kimeenda kwa halali kabisa.

Nawatakia maisha yenye heri na barala Wakili msomi Derick na mke wake Sellen mwenyewe anasema mwenye mwanya, haya kama huna mwenye mwanya elekea ka jiwe.

Leave A Comment